Tuesday, August 9, 2011

WATU 60 WAFA MAJI KATIKA AJALI MBAYA ILOTOKEA VISIWANI COMORO

Takriban zaidi ya watu 60
wakiwemo watoto
wanasadikiwa kuwa wamekufa
baada ya meli ndogo ya abiria
kuzama katika visiwa vya Comoro mapema leo jumanne.
Maafisa wa Comoro wanasema
idadi ya vifo inaweza
kuongezeka katika ajali hiyo ya
meli iliyokuwa na abiria 100.
Haijafahamika haraka chanzo cha
kuzama boti hiyo .
Tayari kundi la uokozi liko katika
eneo la tukio katika bahari
iliyochafuka.
Comoro inavisiwa vitatu kutoka
ufukwe wa msumbiji. Meli hiyo
ilikuwa inasafiri katika kisiwa
kikubwa cha Grande Comore na
kisiwa cha Anjouan.
Lakini shirika la habari ya
kimataifa Reuters limemnukuu
mwendesha mashtaka wa umma
Soilih Mahmoud akisema kuwa
meli hiyo ilikuwa inatokea mji
mkuu wa Moroni kwenda kisiwa
cha Anjoun na kugonga mawe
takriban kilomita tatu nje ya
ufukwe wa kisiwa kikubwa na
kupelekea boti hiyo kuzama .
Shirika hilo linasema miili ya
watu 60 imepatikana lakini
mingine bado imekwama na
itaweza kuondolewa pale bahari
itakapotulia.
Baadhi ya watu walionusurika
waliweza kuogelea mpaka eneo
salama.
Nalo shirika la msalaba
mwekundu linasema watu
wengine walionusurika
walipelekwa katika hospitali za
Ouzioine na Foumbouni.

No comments:

Post a Comment