Wednesday, August 15, 2012

China Bans Muslims from Fastingduring Ramadan

Beijing: China has banned Muslims in the northwestern province of Xinjiang from fasting during the month of Ramadan. The government says the move is motivated by health concerns, but others say it is a campaign to secularize the Muslim minority that can spread violence. Guidance posted on several government websites called on Communist Party leaders to restrict Muslim civil servants, students and teachers from observing fast, visiting mosques and performing other relihious activities during the holy month. The statement posted on the Xinjiang government website urged party leaders to bring “gifts” of food to local village leaders to ensure that they were eating during Ramadan. A statement from Zonglang township in Xinjiang’s Kashgar district said that “the county committee has issued comprehensive policies on maintaining social stability during the Ramadan period. “It is forbidden for Communist Party cadres, civil officials (including those who have retired) and students to participate in Ramadan religious activities,” said the statement. There is “a much more public and concerted effort” than in previous years and in some cases Communist Party leaders are delivering food to village elders to try to get them to break their fast, according to Dru Gladney, a professor of anthropology at Pomona College in California and an expert on China’s Muslim minorities. Regional spokeswoman Hou Hanmin was quoted in the state-run Global Times newspaper Friday as saying authorities encourage people to “eat properly for study and work” but don’t force anyone to eat during Ramadan. Xinjiang is home to about nine million Uighurs, largely a Muslim ethnic minority, many of whom accuse China’s leaders of religious and political persecution. Long- simmering resentment among Uighurs over rule by China’s Han majority and an influx of migrants has sporadically erupted into deadly violence that claimed 200 lives in July 2009. World Uyghur Congress, an exiled rights group, warned the policy would force “the Uighur people to resist against the Chinese rule even further.” “By banning fasting during Ramadan, China is using administrative methods to force the Uighur people to eat in an effort to break the fasting,” said Al-Jazeera has quoted group spokesman Dilshat Rexit as saying.

Monday, August 13, 2012

Iran earthquake relief effortsbegin after 250 killed

Relief operations are under way in Iran after two strong earthquakes in the north- west left at least 250 people dead and more than 2,000 injured. The 6.4 and 6.3 quakes struck near Tabriz and Ahar in in East Azerbaijan province on Saturday afternoon, followed by dozens of aftershocks. More than 100 villages suffered damage - thousands of people spent the night in emergency shelters or in the open. Relief agencies are providing survivors with tents, bread and drinking water. The BBC's Mohsen Asgari in the capital Tehran says hundreds of people were rescued overnight, but that the aftershocks had made the operation exhausting. By midday on Sunday, Deputy Interior Minister Hassan Ghadami said that "all those under debris have been rescued and the quake-stricken people are now being provided with their basic needs". Our correspondent says the operation could be completely quickly because villagers knew each other well so knew where to search, and because the houses were small. 'Mass grave' The towns of Haris and Varzaqan were also among those hit and one resident of Tabriz told the BBC: "The quake has created huge panic among the people. Everyone has rushed to the streets." But local officials said all the deaths have been in rural areas, not in the main towns and cities. The official Fars news agency reported that about 110 villages had been damaged. At least were four totally flattened and 60 others sustained extensive damage. "This village is a mass grave," said Alireza Haidaree, who had been searching for survivors in Baje Baj village. "There are so many other villages that have been completely destroyed," he told AFP. Reports said rescuers attempting to contact remote villages had to do so by radio as many phone lines were cut off.

Uraiqat ataka Palestinaitambuliwe rasmi UN

Mamlaka ya Ndani ya Palestina imeitaka jamii ya kimataifa kuunga mkono uwanachama wa Palestina kama nchi huru katika Umoja wa Mataifa. Saeb Uraiqat kiongozi wa timu ya mazungumzo ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina leo ameitaka jamii ya kimataifa kuunga mkono ombi litakalowasilishwa tena na PLO, la kutaka Palestina iwe nchi mwanachama inayojitegemea katika Umoja wa Mataifa. Huku akiashiria kwamba nchi nyingi za Kiarabu na Kiislamu zinaunga mkono kutambuliwa rasmi Palestina kama nchi huru, Uraiqat amesisitiza kuwa, Mamlaka ya Ndani ya Palestina itaendelea na jitihada zake za kufanikisha suala hilo licha ya mashinikizo mengi yanayoikabili. Mwaka uliopita Mahmoud Abbas Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina alitoa pendelezo la kutambuliwa rasmi nchi huru ya Palestina kwa Ban Ki Moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa lakini kutokana na uungaji mkono wa Marekani kwa Israel na ushawishi wa tawala hizo kwenye umoja huo, pendekezo hilo halikupitishwa.

Tanzania Vs Malawi

MGOGORO wa siku nyingi wa mpaka katika Ziwa Nyasa baina ya Serikali ya Tanzania na Malawi umeibuka kwa kasi baada ya kuwa umetulia kwa muda mrefu. Akiwa Bungeni hivi karibuni kuwasilisha hotuba ya wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2012/13, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Bw. Bernard Membe, aliionya nchi ya Malawi kusitisha shughuli za utafiti wa mafuta na gesi katika ziwa hilo. "Serikali iko tayari kulinda mipaka kwa gharama yoyote ile na inaitahadharisha Serikali ya Malawi kuondoka mara moja na kusitisha shughuli zozote zile za utafiti ndani ya Ziwa Nyasa ndani ya nyuzi 11 hadi 9, kwani sehemu hiyo ni mali ya Tanzania," alisema Bw. Membe. Bw.Membe aliongeza kuwa Tanzania itakuwa tayari kutumia gharama zozote kulinda mipaka yake na kuitaka Malawi kuacha mara moja kuendelea kutoa vibali kwa kampuni zinazofanya utafiti wa mafuta na gesi. Eneo hilo la mwambao wa Ziwa Nyasa, Bw. Membe alisema, linatumiwa na wakazi zaidi 600,000, ambao maisha yao ya kila siku yanategemea ziwa hilo, hivyo kamwe Serikali haitakubali kuona wananchi wake wakinyanyasika. Kwa upande wake, Mwanasheria Mkuu wa Tanzania, Jaji Frederick Werema alinukuliwa na 'Daily Times' la Malawi akimjibu Mbunge wa Mbeya (Vitu Maalum), Bi. Hilda Ngoye, akisema, ÒHatutaki Watanzania waombe ruhusa kutoka Malawi kuchota maji au kuvua Ziwa Nyasa. Kama hatufikii makubaliano tunalipeleka suala hili kwenye sheria za kimataifa.Ó Bi. Ngoye alidai kwamba watalii wa Malawi na boti za uvuvi zimekuwa zikiingia kwenye eneo la maji ya Tanzania kadri wanavyotaka. âÓWatanzania wanaoishi kuzunguka Ziwa Nyasa wanahaki ya kuvua na kufanya shughuli nyingine za uzalishaji katika ziwa hilo, bila kupewa vitisho,Ó Bi. Ngowe aliliambia Bunge la Tanzania, akitaka maelezo kutoka Serikalini kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi. Kwa upande wake, mwandishi Bw. Cedrick Ngalande wa gazeti la 'Malawi Times' la Agosti 6,2012 aliandika katika maoni yake akidai kwamba wakati wa Uhuru watu wachache nchini Tanzania walitaka kumega sehemu kubwa ya Ziwa Malawi (Ziwa Nyasa) kama wanavyoliita wenyewe. Alisema wakati wa enzi za utawala wa Dkt Kamuzu Banda, Tanzania haikuwahi kuzungumzia wazo la kuligawa ziwa na suala hilo lilikuwa karibu limesahaulika kabisa wakati wa utawala wa Dkt. Bakili Muluzi na hata baadaye. Aliendelea kuhabarisha kwamba marehemu Dkt. Bingu wa Mutharika aliipa jukumu kampuni moja kuanza kazi ya utafutaji mafuta katika ziwa hilo na Tanzania haukusema lolote wakati huo na ndicho chanzo cha kuibuka mgogoro huo. "Sasa tuna Rais mpya na ghafla Watanzania wanataka kwamba Serikali iache kufanya shughuli zote za utafutaji mafuta katika ziwa hili mpaka masuala yote yanayohusiana na mipaka yametolewa ufafanuzi. Kwa nini iwe sasa? Alihoji Bw. Ngalande. Bw. Ngalande alisema wakati Bi. Joyce Banda alipotwaa madaraka ya urais, ilionekana kwamba Malawi sasa itatekeleza kila kitu anachoagizwa kufanya Bi. Banda na Jumuiya ya Nchi Hisani. Mwandishi huyo alisema baadhi ya magazeti ya Uingereza yalishangazwa sana na hali hiyo kiasi cha kuwaita watu wa Malawi ÓTaifa linaloogopa wafadhiliÓ. Alisema Rais Joyce Banda aliwahi kwenda London na hata kumpigia magoti Malkia Elizabeth, ambayo ni ishara ya ajabu sana na ukitilia maanani wote wawili ni wakuu wa nchi. "Sawa, maneno yote haya na matendo ukiyajumuisha pamoja yanatoa picha ya uongozi dhaifu wa Malawi. Dunia imenusa harufu ya damu. Sasa Tanzania imeamua ni wakati wa kuligawa ziwa. Kumbuka kwamba hawakulileta wazo hili wakati Bw. Muluzi au Bw. Mutharika walipokuwa madarakani," alisema Bw. Ngalande. "Kama tutaipa Tanzania heshima kusikiliza ombi lake, mtu atashangaa ni kitu gani kitakachofuata baadaye. Je, sasa watadai Chitipa (wilaya ya kaskazini mwa Malawi)? Je, Msumbiji nayo itadai Mlima Mulanje ni wa kwake? Bw. Ngalande aliendelea kuhoji. "Serikali ni lazima iweke wazi kwamba hakuna sehemu yoyote ya Malawi ifanyiwe mjadala Òkwisha!Ó Sasa ni wakati wa kuonesha uwezo wetu. Iambie Tanzania kwamba Ziwa Malawi siku zote lilikuwa, limekuwa na litakuwa la Malawi," aliandika katika maoni yake. "Cha kushangaza, baada ya maelezo yote haya ya kiburi cha Serikali ya Tanzania, jibu la Serikali yetu (Malawi) limekuwa hafifu. Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje (Malawi) ametoa kauli akisema suala hilo litatatuliwa ÓkirafikiÓ. "Kweli, Mhe. Waziri? Nini maana ya maelezo ya kirafiki? Je, unapanga kuligawa ziwa na kuipa heshima Tanzania kwa matakwa yasiyokuwa na msingi? Utawezaje kuwa na utatuzi wa amani kwa madai yasiyokuwa ya msingi? Alihoji zaidi Bw. Ngalande. Kwa upande wake, Bw. Patrick Kabambe, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Malawi alinukuliwa na gazeti la 'Daily Times' la Malawi. Bw. Kabambe alitoa kauli ya ajabu akisema, ÒMadai yetu yako wazi juu ya suala hili. Kwa mujibu wa makubalinano ya ecoland 1890 kati ya Serikali ya Uingereza na Ujerumani, mpaka baina ya Malawi na Tanzania ni kuanzia mwanzo wa maji ya Ziwa Malawi upande wa Tanzania. Kwa hiyo, tunalifahamu fika na tutaendelea kuihusisha Tanzania kama majirani zetu wema.Ó Mgogoro ni kuhusu nani anastahili hasa kumiliki Ziwa Malawi kama linavyojulikana na Wamalawi wengi na Lake Nyasa kama linavyojulikana na Watanzania wengi. Kwa mujibu wa Malawi, hili sio suala la kufanyiwa mjadala. Malawi wakidai wanamiliki asimia 100 ya Ziwa Malawi na kama wataenda kwa mtazamo wa baba yao wa taifa, Dkt. Hastings Kamuzu Banda, Malawi kama ilivyokuwa ikijulikana, Maravi Kingdom, inaweza kutanuka mpaka baadhi ya maeneo ya Tanzania na hata Msumbiji. Kwa mujibu wa Tanzania kwa upande mwingine, ziwa hilo linatumiwa kwa pamoja na mpaka wa nchi hizi mbili unapaswa kufuata mstari wa 'median' katika Ziwa Nyasa. Huu ndio umekuwa msimamo wa Serikali ya Tanzania na shughuli yoyote itakayofanywa na Malawi kupita mstari huu itachukuliwa kama Òkuingia eneo lisilo lakeÓ. Kihistoria mgogoro huu unaanzia Mkutano wa Berlin na tatizo lipo kwenye Sheria ya Bunge la Berlin ya 1885, iliyosainiwa na mataifa 13 yenye nguvu ya Ulaya yaliyohudhuria mkutano huo wa Kuigawa Afrika. Kinyang'anyiro cha kuigawa Afrika Kwa mujibu wa hati za kugawa mpaka kuzunguka Ziwa Nyasa na kusimamiwa na mkataba wa nchi zinazozungumza lugha ya Kiingereza na Ujerumani tarehe 1, Julai, 1890, Dkt Banda mwaka 1962 aliwahi kudai kwamba sehemu moja ya Msumbiji ilipaswa kuwa ya Malawi, wakati huo ikiitwa Nyasaland. Tanzania nayo inaweza kuonesha ramani zinazoonesha mstari wa 'median' kama mpaka na ramani hizo hazijawahi kwenda kinyume na yaliyomo katika mkataba huo. Mgogoro wa Ziwa Nyasa utakuwa vigumu kufutika siku yoyote hivi karibuni kwa pande zote mbili za Tanzania na Malawi na kabla hata ya Uhuru. Mtu anaweza kushangaa kama Watanzania ni wendawazimu kudai nusu ya ukubwa wa ziwa ambapo waliotengeneza ramani hizo wanaonesha mstari wa 'median' kama mpaka. Kuna baadhi ya mikataba ya kimataifa inayoshughulika na haki zinazohusiana na maji. Kutokana na maelezo ya Bw. Patrick Kabambe, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Malawi, ufumbuzi wa suala hili bado ni mgumu. ÒBila shaka, tulifanya majadiliano ya mpaka na tukawaambia Watanzania kwamba kwa jinsi tunavyoelewa, ziwa lote ni mali ya MalawiÓ alisema Bw. Kabambe. Ushauri umetolewa kwamba pande zote mbili za mgogoro huo zinapaswa kukutana na kufikia makubaliano kwa amani. Dkt. Hastings Kamuzu Banda aliwahi kusema, Òsisi sote ni ndugu ramani na mipaka tuliwekewa na wakoloni, kwa hiyo, sisi sote (Wamalawi na Watanzania) tuvue samaki na kuogelea pamoja katika ziwa zuri la Nyasa." Tanzania imekuwa na uzoefu mkubwa ukilinganisha na Malawi katika medani za kivita. Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limeshiriki mapigano mengi kwa mafanikio makubwa ikiwemo oparesheni dhidi ya wakoloni wa Kireno 1960 nchini Msumbiji. Kama hiyo haitoshi, JWTZ iliwahi kupigana dhidi ya majeshi ya Rhodesia na Afrika ya Kusini (1975-1980) na dhidi ya magaidi wa RENAMO wa Msumbiji 1986-1988. JWTZ iliwahi pia kutoa kipigo kitakatifu katika vita ya Kagera 1978 dhidi ya majeshi ya nduli Iddi Amin wa Uganda, ambapo nduli huyo aliweza kuitoroka nchi yake na kuishi uhamishoni mpaka mauti yalipomkuta. JWTZ pia imeshiriki usimamizi wa kulinda amani pamoja na Majeshi ya Umoja wa Mataifa nchini Liberia, eneo la Darfur nchini Sudan na nchi ya Lebanon.

Sunday, August 12, 2012

ULIMBOKA AREJEA NCHINI AKIWA FITI

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Steven Ulimboka amerejea nchini jana akitokea Afrika Kusini alikopelekwa kwa matibabu na kusema amepona kabisa. Ulimboka, ambaye alikuwa anaratibu migomo ya madaktari iliyofanyika mara mbili mfululizo, alitekwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Jumatano ya Juni 27, mwaka huu na kupelekwa katika msitu wa Pande, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, ambako aliteswa na kujeruhiwa vibaya. Katika tukio hilo, daktari huyo aling’olewa meno mawili na kucha za mkono mmoja na baadaye kulazwa katika Kitengo cha Wagonjwa Wanaohitaji Uangalizi Maalumu (ICU) katika Taasisi ya Mifupa (MOI) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH). Baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya, Juni 30, mwaka huu, alisafirishwa kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya vipimo na matibabu. Dk Ulimboka aliwasili jana saa nane mchana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), akitembea mwenyewe na kulakiwa na mamia ya wananchi wa Jiji la Dar es Salaam, wakiwamo madaktari wenzake pamoja na wanaharakati. Huku akibubujikwa na machozi pamoja na ndugu zake, madaktari na wanaharakati nao walimpokea kwa machozi kisha walimkinga kiasi ambacho kulitokea vurugu za kila mmoja kutaka kumwona. Akizungumza kwa ujasiri huku akizongwa na madaktari pamoja na wanahabari, Ulimbona alianza kwa kuwashukuru wote waliofika kumpokea na pia kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kufikisha katika hali aliyonayo sasa pamoja na Chama cha Madaktari waliosaidia kupata fedha za matibabu. Alisema kwa sasa afya yake imeimarika na amepona kabisa na yuko tayari kufanya jambo lolote bila utata na kuruhusu maswali kwa wanahabari, lakini madaktari wenzake walikataa na kumtaka aende kwenye gari ili aondoke kwenda kupumzika. Alitii agizo hilo na kuondoka kwenda kwenye gari. Awali, kabla Dk Ulimboka hajawasili JNIA, nje ya uwanja wa ndege madaktari pamoja na wanaharakati walisikika wakiimba nyimbo mbalimbali zikiwamo za ‘Tanzania Nakupenda, ‘Kama siyo juhudi zako Nyerere’ pamoja na kuhamasishana kuwa Solidarity Forever (Mshikamano Daima). Baada ya kutembea hatua chache na kufika lilipokuwa gari lililombeba, Dk Ulimboka alisimama na kutaka kuzungumza jambo na wanahabari, lakini madaktari na nduguze walimkataza tena na kudai wamuache ili aende kupumzika. Katibu wa Jumuiya hiyo ya Madaktari, Dk Edwin Chitage akizungumzia gharama za matibabu ya Dk Ulimboka, alisema wanazikusanya na kujumlisha na watazieleza hivi karibuni kwa vyombo vya habari. Wanaharakati waliokuwapo uwanjani hapo, walizungumzia kurejea kwa Dk Ulimboka na kudai mapambano yameanza upya, kwani kilichomfanya daktari huyo kupigwa ni kupigania maslahi ya Watanzania wote. Mwenyekiti wa Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA), Ananilea Nkya alisema umefika wakati wa Watanzania kusimama na kuacha woga na unafiki katika kupigania haki za afya zao. Nkya alisisitiza kuwa mapambano aliyoyaanzisha Dk Ulimboka yanaendelea. Jambo lililoungwa mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Usu Malya alisema mapambano ya Dk Ulimboka ni ya Watanzania wote, hivyo kila mmoja anatakiwa kumuunga mkono. Dk Ulimboka alitekwa na kuumizwa vibaya wakati mgomo wa madaktari nchini ukiwa unaendelea, na tangu wakati huo baadhi ya wanasiasa hasa wa upinzani, na wanaharakati wamekuwa wakiituhumu Serikali kuhusika katika kutekwa na kupigwa kwa daktari huyo. Hata hivyo, Serikali kupitia kwa Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, mara kadhaa baada ya tukio hilo, imesisitiza kuwa haihusiki na unyama huo, na wala haikuwa na sababu ya kufanya hivyo. Tayari raia wa Kenya, Joshua Mulundi (21) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, akituhumiwa kumteka na kufanya jaribio la kumwua Dk Ulimboka.

MJUSI ALIYEPELEKWA UJERUMANI KUREJESHWA NCHINI

SERIKALI ina mpango wa kumrudisha nchini mjusi maarufu aina ya Dinosaur aliyechukuliwa mkoani Lindi zaidi ya miaka 100 iliyopita na kupelekwa Ujerumani anakokadiriwa kuiingizia nchi hiyo zaidi ya Dola za Marekani bilioni tatu kwa mwaka, sawa na karibu Sh trilioni tano. Hayo yalisemwa bungeni juzi na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alipozungumzia mikakati ya serikali katika kukuza utalii nchini. Nyalandu alisema Serikali itazungumza na Serikali ya Ujerumani juu ya suala hilo na kwamba, kama atarudishwa, atapelekwa mkoani Lindi. Aidha, alisema kama hilo litashindikana wataangalia pia uwezekano wa kupata asilimia fulani ya fedha inayotokana na watalii wanaomiminika kumuona mjusi huyo. “Katika mambo ya Kale, kuna hili la Mjusi wetu maarufu kama Dinasour ambaye taarifa tulizonazo anaipatia Ujerumani dola bilioni tatu kwa mwaka… huyu alichukuliwa Lindi na wakoloni wa Ujerumani akapelekwa iliyokuwa Berlin Mashariki… tunataka tumrudishe nchini, tutazungumza na Ujerumani… “Lakini niwahakikishie wabunge na Watanzania, tutawashirikisha wadau ili tujue sera na mtazamo wetu kama taifa kuona tutakavyoamua kuzungumza na Ujerumani tuamue kuomba mjusi wetu arudi tumweke Lindi au abaki huko huko, lakini tugawane mapato,” alisema. Masalia ya mifupa ya mjusi huyo, yalipatikana mwaka 1912 huko Tendaguru, Kata ya Mipango katika Jimbo la Mchinga, mkoani Lindi. Amehifadhiwa katika Makumbusho ya Humbolt huko Ujerumani. Nyalandu alikiri kuwapo kwa changamoto nyingi katika kukuza utalii, lakini Serikali imejipanga kufanya kazi kwa kasi ili kuhakikisha yanafanyika mapinduzi makubwa katika sekta ya utalii ili ulinufaishe taifa. Alisema “Hali ya utalii nchini hairidhishi na wizara yangu imeazimia kufanya mabadiliko makubwa. Nchi yetu inapata watalii wachache tofauti na fursa tulizonazo. Dhamira ya Serikali ni kuona nchi inapata watalii milioni mbili kwa mwaka ifikapo mwaka 2015. Kwa sasa, watalii hawafiki milioni moja kwa mwaka.” Alisema mikakati hiyo itakwenda sambamba na kuongeza kasi ya ujenzi wa hoteli na nyumba za kulala wageni ili kuwa na uhakika wageni watakaokuja nchini hawakosi makazi. Nyalandu alisema mikakati pia inafanywa kuboresha mazingira ya viwanja vya ndege, akitolea mfano Uwanja wa Ndege wa Mwanza utapandishwa hadhi na mpango wa kuufanya kuwa wa kimataifa zaidi, utabadilishwa jina na kuitwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Serengeti.

Waislamu wa Myanmar wazidikuteseka

Ripoti mbalimbali kutoka Myanmar zinasema kuwa maafa makubwa yanatokea katika kambi ya wakimbizi wa Kiislamu katika jimbo la Rakhine. Kanali ya televisheni ya Press imeripoti kuwa watu karibu 20 wakiwemo watoto wadogo wamefariki dunia katika kambi hiyo ya Waislamu wa jamii ya Rohingya huko Myanmar kutokana na ukosefu wa dawa na chakula. Ripoti hiyo inasema vijiji kadhaa vya Waislamu wa kaskazini magharibi mwa Myanmar vimeteketezwa kwa moto na Mabudha wanaosaidiwa na jeshi la polisi, na wakazi wa vijiji hivyo wamelazimika kuwa wakimbizi. Mabudha hao wenye misimamo mikali pia wamechoma moto misikiti kadhaa. Umoja wa Mataifa umesema kuwa ukatili wanaofanyiwa Waislamu wa Myanmar ndiyo mkubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa duniani katika siku za hivi karibuni. Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch (HRW) limesema kuwa jeshi la Myanmar limetenda jinai nyingi dhidi ya Waislamu wa Rohingya walio wachache. Ripoti hiyo imefafanua kuwa miongoni mwa jinai hizo ni kubakwa wanawake wa jamii hiyo ya Waislamu kaskazini mwa Myanmar.

Wakenya 13 wafariki dunia katika ajali ya mabasi ilotokea tanzania

Idadi ya watu walofariki katika ajali ya mabasi mawili karibu na mji wa Tanga Tanzania Ijuma asubuhi imefikia 13. Watu 42 wamejeruhiwa miongoni mwao 14 wako katika hali tabani, watu 29 hawakujeruhiwa. Walofariki ni miongoni mwa kundi la wanawake wa Kenya kutoka kanisa la Presbyterian Church of East Africa - PCEA kutoka Thika walokuwa wanasafiri kuelekea Dar es Salaam kwa sherehe za kidini Tanzania. Kamanda wa polisi wa mkoa wa Pwani Tanzania, Ernest Mangu ameiambia sauti ya Amerika kwamba serikali ya Kenya inashirikiana kwa karibu sana na Tanzania na imepeleka ndege maalum kuwasafirisha nyumbani walonusurika.

MISRI YATUMA VIKOSI VYAKE SINAI

Misri imetumia Helicopter kufanya mashambulizi ya mizinga dhidi ya wakereketwa wenye imani kali walio katika eneo la Sinai tangu mwaka 1973 katika kile jeshi la Misri lililochotaja kama shambulio la kurejesha utulivu. Matumizi ya anga ni ishara ya mabadiliko ya vita vya Misri dhidi ya wakereketwa wa Kiislam ambao wamezidisha shughuli zao katika eneo lenye milima na jangwa lenye mpaka na Israili na Gaza. Mapema wiki hii wapiganaji wakereketwa waliishangaza Misri kwa ujasiri wao kwa shambulizi ambamo askari 16 waliuawa, magari ya jeshi yakaibwa na kuelekea Israel kwa lengo la kujaribu kufanya shambulio jingine. Katika taarifa iliyosomwa kwenye televisheni ya taifa jeshi limesema kua limeanzisha operesheni ya mchanganyiko wa vikosi kwa kutaka kurejesha utulivu huko Sinai, majeshi yakiungwa mkono na Jeshi la anga. Shambulio la siku ya jumapili ndio baya kuwahi kufanywa huko Sinai kwa miaka mingi na hatari kuliko yote dhidi ya vikosi vya Misri ikiashiria ongezeko la vitendo vinavyokiukaq sheria katika eneo hilo. Katika tukio la hivi karibuni, watu wenye silaha waliwafyatulia risasi walinzi kwenye vizuizi huko El -arish, mji mkuu wa Wilaya ya Sinai, mji ulio umballi wa kilomota 50 kutoka mpaka wa Gaza na Israili. Ghasia kwenye mpaka wa Israel na Misri inaweza kutishia mkataba wa amani baina ya nchi hizi mbili. Hio ndio sababu Israel imeiambia Misri ichukue hatua za kusuluhisha vurugu badala yake kupeleka vikosi vyake. Israel imekubali kuondoa baadhi ya masharti yanayozuwia shughuli za kijeshi katika Sinai ili Wa Misri waweze kuingiza vikosi zaidi. Lakini uvamizi wa Misri dhidi ya kile walichokiita magaidi hautobadili lolote katika sehemu ya Sinai inayokaliwa na makabilia ya Wa Bedwini wenye fikra huria. Ni eneo linalovutia kwa makundi ambayo yangependa kutumia sehemu isiyokua na utaratibu wowote wa uongozi kwa aijili ya kuifika Israili.Rais wa Misri Mohammad Mursi aliahidi kwamba atadhibiti eneo la Sinai kwa ukamilifu.

Wednesday, August 8, 2012

Amnesty Internationallazionya pande zinazopiganakwenye mji wa Aleppo nchiniSyria kuacha kutumia silahanzito dhidi ya raia

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu duniani la Amnesty International limeonya dhidi ya kuendelea kutumika kwa silaha nzito kwenye mji wa Aleppo kati ya wanajeshi wa Serikali na waasi wa jeshi huru la Syria. Picha mpya za satelite zimeonesha kuongezeka kwa matumizi makubwa ya silaha nzito kwenye mji wa Aleppo na kuendelea kuzusha hofu kuhusu hali ya usalama wa wananchi ambao wamenaswa kwenye mji huo. Wanaharakati nchini humo wamedai kuwa wamegundua zaidi ya mashimo makubwa 600 yanayoonekana kwenye mji wa Aleppo yamesababishwa na kutumika kwa silaha nzito kwenye makazi. Shirika la Amnesty International limesema kuwa pande zote mbili zinazopigana kwenye mji huo zinawajibika kutokana na kile kinachoshuhudiwa na matatizo ambayo wananchi wanakumbana nayo wakati mapigano hayo yakiendelea. Hapo jana waangalizi wa Umoja wa Mataifa UN waliamua kuondoka kwenye mji huo kwasababu za kiusalama baada ya kuongezeka kwa mashambulizi ya anga yanayofanywa na majeshi ya Syria. Juma hili ujumbe maalumu wa Iran umesafiri hadi mjini Damascus kukutana na rais Bashar al-Asad, ujumbe ulioongozwa na mpatanishi wake Saeed Jalili ambaye anakutana kwa mara ya pili na utawala wa Syria. Ujumbe huo uko nchini Syria kujaribu kushawishi kundi ambalo linawashikilia raia wake zaidi ya 48 ambao liliwateka jumapili iliyopita wakiwa njiani kuelekea uwanja wa ndege. Waasi wa Syria wamekuwa wakiituhumu Serikali ya Iran kwa kuendelea kuiunga mkono serikali ya Asad ambayo wamedai ni haramu na katili kwa kuendelea kuwaua wananchi wasio na hatia. Hii leo waziri wa mambo ya nchi za nje wa Iran Ali Akbar Salehi amesema miongoni mwa raia wake waliotekwa mmoja kati yao ni mwanajeshi mstaafu wa jeshi la nchi hiyo.

Marekani yataka Rwanda kusitisha Msaada kwa Waasi wa M23

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton ameitaka serikali ya Rwanda kuisaidia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kuwanyang'anya silaha waasi wa M23 na kusitisha msaada kwa Kundi hilo kwa lengo la kupata suluhu ya mgogoro wa Mashariki mwa nchi hiyo. Clinton amesema wanataka kuona nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR zinashiriki kikamilifu katika kurejesha usalama nchini DRC na kulisambaratisha Kundi la Waasi la M23 ambalo linatekeleza mashambulizi Mashariki mwa nchi hiyo. Kauli hii inakuja kipindi hiki ambacho Viongozi kutoka nchi kumi na moja za Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR wakiwa kwenye mkutano wa siku mbili nchini Uganda kujadili usalama wa DRC ili kulimaliza Kundi la M23. Clinton ametaka Viongozi hao wa Ukanda wa Maziwa Makuu kutathimini kwa kina namna ya kuweza kushughulikia mgogoro huo na hatimaye kurejesha utulivu ambao umepotea Mashariki mwa DRC. Mkutano wa Viongozi wa Nchi za Maziwa Makuu ICGLR umeingia siku ya pili ambapo Rais wa DRC Joseph Kabila Kabange hatukutana tena na Rais wa Rwanda Paul Kagame kama ambavyo ilipangwa awali na badala yake wataandaliwa kikao chao pekee. Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Oriem Okello amesema Viongozi hao wawili hatokutana na badala yake Rais Yoweri Kaguta Museveni ataandaa mkutano baina yao na kwa sasa wamejiegemeza kujadili kupata Jeshi litakalolinda amani mpaka mwa DRC. Viongozi wa Nchi za Maziwa Makuu ICGLR wataamua Kikosi ambacho kitaenda kulinda mipaka ya DRC na kukabiliana na uasi ambao unafanywa na Kundi la Waasi la M23 ili kusaidia juhudi za amani. DRC yenyewe imeshaainisha haitaki nchi ya Rwanda ishirikishwe kwenye Jeshi hilo kutokana na kudaiwa kuwafadhili Waasi wa M23 huku Kigali yenyewe ikishinikiza inataka kushiriki kwenye mpango wa kurejesga amani. Katika hatua nyingine Mkuu wa Shirika la Misaada ya Kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA Valerie Amos anaendelea na ziara yake kuangalia madhara ya mashambulizi ya Kundi la M23 nchini DRC. Amos amesema hali ni mbaya Jimboni Kivu kitu ambacho kama hakijadhibitiwa kinaweza kuzua maafa zaidi kwa wananchi wa eneo hilo kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara ambayo yamekuwa yakifanywa na Kundi la Waasi la M23. Kundi la Waasi la M23 limeendelea kujigamba kupiga hatua kwenye mapambano yake na Jeshi la Serikali hasa katika maeneo ya Rutchuru na sasa wanaendelea kusaka uungwaji mkono kutoka kwa wananchi.

Tuesday, August 7, 2012

MALAWI Vs TANGANYIKA( TANZANIA BARA )

Malawi imekataa kuitikia wito wa Tanzania kutaka isimamishe shughuli za kutafuta mafuta na gesi ziwa Malawi, wakati suluhu ya mvutano wa mpaka ikisubiriwa. Mvutano wa maneno umezuka kati ya nchi hizo mbili baada ya Malawi kuipa leseni Kampuni ya Uingereza kufanya utafiti katika eneo hilo. Maafisa nchini Tanzania wanasema mvutano huo uliodumu kwa miaka 50 sasa unaweza kuwa mkubwa iwapo ugunduzi wa mafuta na gesi utatokea kwenye ziwa hilo linalojulikana kama Ziwa Nyasa nchini Tanzania. Tanzania inasema inaendelea kufanya mazungumzo na Malawi na iko Tayari kulipeleka suala hilo kwenye vyombo vya upatanishi. "Hili ni suala nyeti sana na tungependa litatuliwe kwa maelewano, tutaendelea na mazungumzo," Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania alisema. Membe wiki iliyopita alviambia vyombo vya habari nchini humo kuwa "shughuli za uchimbaji katika eneo la kaskazini mashariki mwa ziwa hazina budi kusitishwa kupisha mazungumzo kutatua mzozo huo yafanyike." Malawi, koloni la zamani la Uingereza, kwa upande wake iliapa kuendelea na chughuli za utafiti wa hewa gesi mkaa (hydrocarbons). Tanzania,lililotawaliwa na Ujerumani na baadaye Uingereza, inadai kuwa sehemu ya kilometa za mraba 29,600 sawa na maili 11,400 za ziwa, wakati Malawi inarejea makubaliano ya mwaka 1890 yanaonyesha kuwa mpaka kati ya nchi hizo mbili uko kwenye ufukwe upande wa Tanzania. Msumbiji pia inadai ina sehemu yake katika ziwa hilo la tatu kwa ukubwa barani Afrika.Mwezi Septemba mwaka jana serikali ya marehemu Bingu wa iliipa leseni kampuni ya Surestream Petroleum, kutafiti mafuta na gesi ziwani. Mataifa hayo mawili yatafanya mazungumzo juu ya mpaka kaskazini mwa Malawi katika mji wa Mzuzu Agosti 20 mwaka huu.

Iran Says Test of Upgraded Short-RangeMissile Was a Success

TEHRAN (AP) - Iran said Saturday that it had successfully test-fired an upgraded version of a short-range ballistic missile with improved accuracy, increasing its capacity to strike land and naval targets. Iran's defense minister, Brig. Gen. Ahmad Vahidi, said the solid-fueled Fateh-110 missile had a range of 185 miles. He also said the weapon could strike with pinpoint precision, making it the most accurate weapon of its kind in Iran's arsenal. "By reaching this generation of the Fateh-110, a new capability has been added to our armed forces in striking sea and land targets," state television quoted General Vahidi as saying. Iran's military leaders have said they believe that future wars will be air- and sea-based, and Tehran has sought to upgrade its air defense systems and naval power in anticipation of such a possibility.

TETESI: MEMBE AKALIA 200BN/= ZA ZANZIBAR

Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na “Ushirikiano wa Kimataifa” amekalia pesa za Zanzibar zipatazo 200bn/= zilizotolewa na wafadhili kwa ajili ya kuipa Zanzibar kuendeleza/kufufua specifically zile EPZ, maeneo huru ya kiuchumi Zanzibar. Waliotoa pesa hizi wakiwemo UAE/Rasil Khemah – ambao viongozi wetu wote watatu (Shein, Seif-1 na Seif-2) wamekuwa kiguu na njia kutafuta misaada. Imepatikana Membe – laatul laah amezuia, just kutia saini tu ili pesa ziwe released. Kipengelea kimoja kinachomfanya Membe ndiye atiwe saini/pesa za misaada, mikopo, zawadi n.k zinapoingia katika foreign currency au misaada kama hiyo – Zanzibar hairuhusiwi kusaini, kwa sababu ‘si nchi’ inatakaiwa TZ ndio imwage wino. Huu ni mwezi wa pili, Membe amekalia barua yetu na pesa zetu, halali yetu. Baadaye wanakuja Zanzibar eti kujiliza baada ya meli kuzama. Hiyo ndio TZ, na huo ndio Muungano wetu uliodumu miaka 48 kwa Bara kuidhulumu Zanzibar. * Plus, jana tu Abubakar alikuwa anasema ndani ya BLW kuwa hao hao akina Membe wameinyima Zanzibar fursa ya kuhudhuria vikao muhimu vya kimataifa kwa kuwanyima wajumbe wake visa, just kwa sababu wao watanganyika hawakwenda au hawakutakiwa kuwemo. Ushauri wangu: MAMBO YA NCHI Z ANJE IONDOSHWE KABISA KATIKA LIST YA MUUNGANO (GET ME RIGHT PLEASE, SIO SUALA LA KUGAWANA MABALOZI, LA HASHA). ONDOA FOREIGN AFFAIRS KATIKA LIST HIYO FOR GOOD. Mbaya zaiid katika sakata hili la Membe kuzuia pesa zetu, naibu wake anaitwa Mahadhi Juma Maalim – mzanzibari wa Muyuni/na Mungoni (huyu ni kambi ya NO vote katika referendum, na ndiye group la akina Samia, Haroun, Shamsi, Perera Ame Silima – wanachochea watu wa kusini wasema NO serikali tatu au muungano wa mkataba). Mahadhi, Kazi ya uzinzi haifai na kutafuta wanawake kuowa. Kuwa na akili wewe, nchi yako inazamishwa. Hizi habari za Membe kukalia 200bn/= zimeigusa BLW na cabinet ya Zanzibar – ni habari zilizoleta ghazab sana, maana hili si la mwaka 1968 au 1980s au 1970s – it’s only two months ago or less (jana na leo). Source mzalendo.net

WAUMINI WA KIISLAMU VISIWANIZANZIBAR WAAMUA KUMUACHIA M/MUNGU ATOE HUKUMU KWA WALEWOTE AMBAO HAWAITAKII MEMAZANZIBAR

Maelfu ya waislamu nchini zanzibar wameamua kujikusanya katika msikiti Afraa ulioko kidongo chekundu kwa ajili ya kumshtakia M/mungu juu ya suala zima la kukashiwa na kufanyiwa vitendo vya uonevu na wale ambao hawaitaki mema nchi ya zanzibar. Mkusanyiko huo ulikua na lengo la kuomba Dua maalum ambayo imeeandaliwa na jumuiya ya muamsho zanzibar kwa lengo la kuwaunganisha waislamu ili wawe kitu kimoja katika kudai na kutetea maslahi ya nchi yao,vile kumuomba mungu awanusuru viongozi wa harakati za kuitakia mema zanzibar na shari za maadui zao, katika dua hiyo kuliambatana na uchinjaji wa wanyama tofati kwa ajili ya sadaka ambayo walipewa mayatima na wanawake. Akibainisha idadi ya vichinjwa hivo amir wa jumuiya hiyo SH FARID HADI amesema jumla ya ngombe saba, mbuzi 33, kondoo 3, kuku 22, bata 1 na njiwa 1 wamekabidhiwa na wamewachinja wote. Kwa upande wao viongozi wa jumuiya ya muamsho wameweza kujichinjia wanyama kwa mikono yao kwa kushirikiana na waumini wengine ambao walibahatika kuwepo katika viwanja vya uchinjaji. Amesema dua hii imeamuliwa kuwekwa mwezi 17 Ramadhan kwasababu tarehe hii ina historia kubwa katika ushindi wa waislamu. kwani siku kama hii ndio siku ambayo Allah aliwanusuru waislamu katika vita vya badri. Aliongeza kwa kusema waisalmu wanatakiwa wawe na umoja wa ukweli ukweli ili kuweza kuwashinda maadui zao na kupata ushindi kwa yale wanayoyahitaji. Nae kwa upande wake sh MSELEM bin ALLY AMEWAOMBA waislamu waendelee na msimamo wao ule ule wa kutokushiriki suala zima la sensa ambayo inategemewa kufanyika hvi karibuni. Source mzalendo.net

Wednesday, August 1, 2012