Tuesday, December 13, 2016

Majambazi waiba dhahabu ya kilo 70 Ufaransa

Majambazi waliokuwa na silaha wameiba dhahabu ya kilo 70 nchini Ufaransa na kutoroka.
Majambazi hao wanne waliokuwa wameabiri magari mawili walishambulia gari la usalama lililokuwa likisafirisha dhahabu hiyo karibu na mji wa Lyon.
Walitumia gari moja kuziba barabara.
Kisha, walichukua dhahabu hiyo inayokadiriwa kwua ya thamani ya €1.5m ($1.6m; £1.3m), na kuipakia kwenye gari moja lao ambalo walikuwa wamepanga kulitumia kutoroka.
Baada ya hapo, waliwafungia walinzi wawili waliokuwa wanasafirisha dhahabu hiyo nyuma ya gari lao kabla ya kuteketeza gari ambalo walikuwa wamelitumia kufunga barabara.
Walinzi hao waliokolewa na maafisa wa polisi baada ya mtu aliyeshuhudia tukio hilo kuwapasha habari.
Wezi hao walitoroka upesi na kuacha moto uliokuwa kwenye gari waliloliwasha moto ukienea na kufikia magari mengine yaliyokuwa karibu ingawa muda mfupi baadaye wazima moto walifika na kuuzima.
Kisa hicho kilitokea katika barabara ya A6 inayounganisha Lyon na Paris.
Polisi wanawasaka wahusika.

No comments:

Post a Comment